ZIARA YA MWANASHERIA MKUU TUNDU LISSU (MB) ULAYA NA MAREKANI Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari ...
Naibu Katibu Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe. John Mnyika akiwa amefatana na Mgombea Ubunge Jimbo la Buyungu pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama kwenye uzinduzi wa kampeni ulifanyika Kata ya Kasnada yenye vijiji vinne huku vijiji vitatu vikiongozwa na wenyeviti wanaotokana na Chama cha Demokrasi na Maendeleo.
Akiongea na wakazi wa Kata ya Kasanda Mhe. John Mnyika aliwashukuru wakazi hao pamoja na wanachi wa Buyungu kwa ujumla kwa kuweza kuchagua Mbunge sahihi aliyekuwa anatokana na CHADEMA na kwa muda aliwatumikia wakazi wa Jimbo hilo ameweza kufanya mambo mengi yanayoonekana kwa jamii ikiwa ni pamoja na Kuanzisha shule ya Sekondari yenye kidato cha tano na sita jambo ambalo hapo nyumba Wilaya hiyo haikuwai kuwa na Shule wa Sekondari, Kugawa gari za kubebea wagonjwa (Ambulance) tatu kwenye Kata ya Nyamtukuza, Kituo cha Afya cha Nyanzige na Kituo cha Afya cha Kakonko.
Akiongea kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Mhe. John Mnyika aliwaomba wakazi wa Buyungu kumuonyesha Rais Magufuli kuwa Chama chake hakiwezi kutawala milele kwa kumkataa Mgombea wake na wamchague Mhe. Elia Fredrick Michael anaetokana na Chama cha Demokrasia na Manednelo ili akasimamie yale yaliyoanzishwa na Marehemu Kasuku Bilago.
Huku akiwataka watendaji wa Serikali kuacha mara moja tabia ya kuwatisha wananchi wanoonekana kuunga mkono vyama vya upinza na amewaomba wanancho kutoa taarifa kwa viongozi wa Chama pale tu wanapoona kunasehemu kunaviashiria vya rushwa au kutishiwa na viongozi hao watalifanyia kazi mapema ili kuepusha kuhujumiwa kwenye uchaguzi huo.
Akielezea sababu za kuwaomba watu Buyungu wamchague Elia ni kutokana na wawakilishi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi kuacha kuwatetea wananchi na badala yake wanalinda maslahi ya Serikali na Chama cha huku wakiwaacha wananchi wakiteseka, akitolea mfano swala la Serikali kuchukua fedha za wakilima wa korosho jambo ambalo lilizua mjadala mkali kwenye vikao vya Bunge na Chama cha Mapinduzi kuwatishia Wabunge wao wanaokataa kuunga mkono swala hilo watafukuzwa uwanchama, hivyo basi basi kumchagua mgombea wa Chama cha mapinduzi ni kuongeza mateso kwa wakazi Jimbo Buyungu.
MGOMBEA UBUNGE
Akiongea na wakazi wa Jimbo la Buyungu kupitia mkutano wa uzinduzi wa kampeni ulifanyika kwenye viwanja vya Kasanda Mgombea Ubunge aliwaomba wananchi wa Jimbo hilo wampe ridhaa ya kuwawakilisha kwenye Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani ili aende kuwatetea paomja na kuwaletea maendelie wakazi wa Jimbo hilo pamoja na Wilaya ya Kakonko.
Mhe. Elia alieleza kazi alizokuwa akizifanya kwa kushirikiana na Mbunge Marehemu Kasuku Bilago yeye akiwa kama Diwani wa Kata ya Gwalama, ni pamoja na kuhakikisha wanasimamia haki na kupigia kelele maovu yanofanya kwenye Halmashauri ambapo Halmashau ya Kakonko ilipitisha Sheria ndogo za kuwataka wakazi wa Wilaya ya Kakonko kuanza kulipia kodi ya majengo jambo ambalo liliwafanya madiwani wa CHADEMA kutoshiriki kikao hicho na kupigia kelele na kupelekea Halmashauri kushindwa kutekeleza lakini na walimfikishia Mbunge Marehemu Kasuku Bilago na akalifikisha kwa Wazir mwenye dhamana na kuwajibu kwa barua kuwajambo hilo lipo kinyume na sheria hivyo halipaswi kutekelezwa kwenye Halmhauri kama ya Wilaya ya Kakonko ambapo wakazi wake wegi ni watu wenye kipato cha chini na alipofariki Mbunge wa Jimbo hilo baadhi ya Kata zinazoongozwa na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi wameanza kukusanya kodi hizo, akihaidi kusimamia haki na maswali ya wananchi Elea aliwataka wkazi wa Buyungu kutolipia kwani.
Akizungumzia swla la Afya Mhe. Elia Fredrick aliwahakikisha wakazi wa JImbo hoo kuhakikisha Kila Kata inapata kituo cha Afya na ahadi hiyo tayari Marehemu alishaanza kufatilia hivyo yeye anakwenda kuendelea pale alipoishia Marehemu Bilago, pamoja na kuimarisha swala la Afya Elia aliwahakikishi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuleta amani kwa wakazi wanaoishi kwenye Kata zilizopo karibu na mipaka ya Nchi jirani.