Be Part of our Chama

Request Details

Habari / Makala Mpya Zaidi

ZIARA YA MWANASHERIA MKUU TUNDU LISSU (MB) ULAYA NA MAREKANI Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari ...

Soma Zaidi

BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA

Baraza la Wazee wa CHADEMA limeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 7.8.1 ya Katiba ya Chama ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2016. Baraza linaundwa na wanachama wa CHADEMA wenye umri usiopungua miaka 50 ya kuzaliwa kwa mujibu wa ibara ya 7.8.2 (c) ya Katiba ya Chama.

Baraza la Wazee linaongozwa na Mheshimiwa Hashim Juma ambaye ni Mwenyekiti na Mheshimiwa Roderick Lutembeka kama Katibu kwa ngazi ya Taifa.

Baadhi ya majukumu ya Baraza ni kama ifuatavyo;

  1. Kutoa ushauri kwa Chama katika ngazi zote
  2. Kutatua na kusuluhisha migogoro ndani ya Chama
  3. Kuwahamasisha Wazee kujiunga na Chama
  4. Kutoa ushauri kwa Chama kuhusu sera, mikakati na mipango inayowahusisha Wazee na wananchi kwa ujumla
  5. Kutetea maslahi ya Wazee ndani ya nchi
  6. Kushauri Chama kuhusu masuala ya kimaadili kwa viongozi, wanachama na wananchi kwa ujumla.

Kauli mbiu ya Baraza la Wazee ni:

“WAZEE”- “HAZINA YA HEKIMA NA BUSARA”

Makao Makuu  ya Baraza yapo Jijini Dar es Salaam na pia tunayo ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Zanzibar.