ZIARA YA MWANASHERIA MKUU TUNDU LISSU (MB) ULAYA NA MAREKANI Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari ...
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akizindua Sera ya CHADEMA toleo la Mwaka 2018, ghafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na taasisi mbalimbali za Kiserikali na Mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya Nchi.
Akiongea na wageni waalikwa Mhe. Freeman Mbowe alieleza kuwa Sera hiyo imegawanyika katika maeneo 12 makuu.
Maeneo hayo ni Katiba, Uatwala ,Uchumi wa soko Jamii, Siasa za ndani, Siasa za Kijamii, Elimu na Sayansi, Afya, Usimamizi wa Ardhi, Kilimo, Miundombinu, Mazingira pamoja na Mambo ya Nje.
Uzinduzi wa sera ulifanyika Jijini Dar es salaama katika ghafla fupi iliyohudhuriwa na wawakilishi wa mabalozi, viongozi wa dini na watu wa kada mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe ambaye alitumia muda mwingi kuzihusianisha sera za chama hicho na mambo aliyokuwa akiyasema Hayati baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere.
Mbowe alisema sera zitakuwa zinafanyiwa marekebisho kulingana na wakati.
Alisema eneo la kwanza lililopo kwenye sera hizo ni lile linalolinda uhura wa wananchi.
Mbowe alisema Mwalim Julius Nyerere aliwai kuzungumzia suala la maendeleo ya watu na uhuru, jambo ambalo wamelijadili kwa kina kwenye sera hiyo.
Alitaja eneo jingine ni nafasi ya kuwa na sera zinazolenga misingi ya uchumi.
Alisema katika eneo hilo waliainisha ni kwa namna gani wananchi watapata huduma za kijamii.
Alifafanua eneo hilo kwa limeainisha namana uchumi utakavyokuwa endelevu badala ya kuwa uliohodhiwa na Serikali.
Mbowe aliitaja sera nyingine zinazoilinda na kuihuisha jamii kupata huduma ya maji, barabara yasiwe mambo yanayofanywa na sekta binafsi bila yanafanywe na Serikali.
“Imejengekea dhana kuwa maendeleo yanaofanywa na Serikali kama kujenga Shule, Zahanati kuwa ni msaada, hii si sawa hayo ni majukumu ya Serikali” Alisema Mbowe.
Mbowe alisema kabla ya kutayarisha sera hiyowametumia mwaka mzima kufanya tafitina kukusanya maoni kutoka kwa watu mbalimbali.
Alisema sera zao ni mjumuiko wa mawazo ya watu wengi kwa muda mrefu wala sio fikra za mtu mmoja, ambayo itawataka wanachama wote kukubaliana na matokeo.
“Chadema ni Chama kinachokuwa, kinavutia wato kutoka makundi mbalimbalikunawatu wanakuja na mawazo mapya na kubadilisha yale ya zamanina kuendeleza mazuri”, Alisema.
Alisema haamini kuwa kuna kiongozi yeyote ambaye anaweza kusema malengo ya Mwalimu Nyerere yalikuwa mabaya kwa Nchi.
Mbowe alisema “Nyerere alikuwa ni kiongozi mwadilifu, na misimamo ya kisera na kiitikadi alikuwa na uwezo na kusimamia kile ambacho anakiamini hata kama pengine baadaye kingepingwa, lakini dhamira ya mwalimu kawa taifa siku zote ilikuwa ni ‘positive’.
Aliongeza kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi aliyeinyesha uadilifu mkubwa na msemakweli ndani na nje ya nchi.
“Hivyo alikuwa ni sifa nayomtofautisha na kiongozi ambaye anataka kujinufaisha kwa maslai yake binafsi, alijitoa kwa moyo wake wote na nguvu zake zote, mambo mengi mazuri yalifanywa na Mwalimu” alisema.
Alisema lazima itambuliwe kuwa utawala wote unakuja na kutoka hata uwe mwema kiasi gani, Mwalimu alikuwa mzuri na alifanya mema hasa katika nyanja ya uchum, utabaki misingi misingi mikubwa ya taifa.
“Taifa linapomnukuu Mwalimu lazima lijiulize linaishi vile ambavyo ameelekeza, imekuwa utamaduni wa wanasiasa wengi kumnukuu Mwalimu lakini ni kwa kiwango kipi tunaishi na kutekeleza yale amabyo ametuwekea?
“Katika ujenzi wa taifa moja ni kwa vipi viongozi aliotuachia waaweza kuhakikisha wanaendeleza umoja huo bila kubaguanakwa imani na kiitikadi.
“kwa hiyo tutakapojadili sera zetu tutarejea kujifunza katika matukio ambayo tumeyapitia katika safari yake kisiasakama chama cha siasa na yakasaidia kutengeneza diara isiyobaguana, inayotambua umuhimu wa masilahi ya kila mtu, tukianza kujadili nchi yetu kuna mambo kama matano ambayo aliyatengeneza mwalimu” alisema.
Vyama vingi vya siasavilianza mwaka 1961-1967 nchini mwetu ingawa, kuna Watanzania wengi wanaamini vyama vingi vya kisiasa vimeanza mwaka 1961 wakati wa uhuruna vyama hivi vilikuwepo hadi mwaka 1975 na mwalimu lijenga mshikamano wa kitaifa kwa Watanzanio wengi.
Alisema kwa kupitia Mwalimu Nyerere kila utawala unakuwa na sera zake, kuna sera ambazo zimekuwa zinamuona kiongozi maskini ndio anayestahili kuongoza, jamabo mabalo limekuwa likifikisha fikra za watu katika kuwa mskini wakati Chadema inatakamani kila mmoja awe tajiri.
“Umaskini sio sifa ni laana, tunahitaji viongozi wanaochukia umaskini na sio wanaohusudu umaskini, unaposema mimi ni kiongozi wa wanyonge, dhana ile inabaki kwa watu kwamba wao ni maskini, kwa hiyo ikitafuta ukapata utajiri kwao wao ni uadui” alisema.
Alisema kuwa Chadema haikubaliani na sera hiyo hivyo sera zao lazima zijikite katika kunyanyua hali za watu watafute mali na Serikali yenyewe iwezeshwe kwa kujenga uchumi wa ncho wao, wanahangaika ili watu wote wawe na ustawi mzuri wa maisha.
“Ujamaa ulisbabisha kuwa na dhana hiyo, hivyo wao Chadema wamaikataa, bila wanahitaji uadilifu wa serikali itengenese mazingira bora, mwalimu alizisifia sera za Chadema wakati huo, hivyo hawawezi kujenga maendeleo kama hawana utaalamu wa kidemokrasia, Chadema sio Chama cha ugomvi kimamapenzi mema na nchi na huwa kinafanya utafuti na kina mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi” alisema na kuongeza.
Uhuru wa watu na sio kwamba kilinda maendeleo ya vitu, sio hizo ndege watu wawe na uhuru na kuwe na uwazi ndipo vitu vingine vije,haki za msingi, katiba.
Toleo la sera hii nimarejeo ya sera ya kwanza ya Chama kilichojipambambanua kuwa na mrengo wa kati iliotolewa mwaka 1993, marejeo ambayo yamezingatia mawazo ya mkutano mkuu wa taifa wa Chama 2015.
Picha baadhi wa jumbbe wa Kamati Kuu wa Chadema wakifatilia hutuba ya Mwenyekiti Taifa
Mhe. Freeama Mbowe wakati wa uzinduzi wa Sera toleo la mwaka 2018
(Picha na Abdulkarim Hussein)
Picha viongozi wa Kuu wa CHADEMA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa na wawakilishi wa Taasisi na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya Nchi kwenye uzinduzi wa sera 2018
(Picha na Abdulkarim Hussein)