Be Part of our Chama

Request Details

Habari / Makala Mpya Zaidi

ZIARA YA MWANASHERIA MKUU TUNDU LISSU (MB) ULAYA NA MAREKANI Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari ...

Soma Zaidi

MHE. GODBLES LEMA AITAKA SERIKALI KURUHUSI WACHUNGUZI WA KIMATAIFA

Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Goodbles Lema mamepma leo amitaka Serikali kuruhusu wachunguzi kutoka nje na kwa kufanya hivyo kutaiondolea Serikali lawama juu ya kutekwa kwa mfanjabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’

Lema aliyasema hayo leo tarehe 16 Octoba alipozungumza na  mkutano wake na wanahabari  Makao Makuu ya CHADEMA Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliitaka Serikali kukubali na kuomba msaada kwenye mataifa ya nje ili waje kusaidia kufanya uchungu kutokana na matukio haya ya utekaji na kuuwawa kwa watu jambo ambao sio kama litailetea aibu Taifa kwani hata mataifa yaliyoendelea huomba msaada pale wanapopata majanga kama hayo.

“Eneo alilotekwa mfanyabiasha Mo Dewji ni eneo ambalo linaulizi mkubwa nashangazwa mpaka sasa hakuna viashiria vya kuonyesha kupatikana kwake ikiwa ni pamoja na kulinganisha juhudi za vyombo vya ulinzi na usalam kuonyesha havipo seriouse  kwa jambo hili” Alisema Lema

Pamajo na kuitaka Serikali  kukubali kupata msaada kutoka mataifa ya nje Mhe. Lema alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. kangi Lugola kuacha mara moja kuwazuia watu kujadili kuhusiana na kutekwa kwa mfanyabiasha Mo Dewji kwani kuwazuia ni sawa na kuwanyima watu kuli kwenye msiba.

Mfanya biashara  Mo Dewji ambaye miaka mitatu iliyopita jarida la Forbes lilimtaka kuwa tajiri namba moja Afrika mwenye umri chini ya miaka 40.

Jana, familia ya Mo Dewji alitangaza zawadi kwa yeyeote yule ambaye atasaidia kufanikisha kupatikana kwa mfanyabiasha huyo zawadi ya Shilingi Billion Moja (1,000,000,000)

Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana siku ya Alhamis, Oktoba 11,2018 majira ya saa 11:30 alfajiri wakati akiwa  Hoteli ya Colesseum na mpaka leo tarehe 16 Oktoba saa 5:30 asubuhi hajapatikana wala kutolewa taarifa yoyoyte juu ya utekaji huo.