ZIARA YA MWANASHERIA MKUU TUNDU LISSU (MB) ULAYA NA MAREKANI Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari ...
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inakutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam katika kikao chake cha kawaida chini ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe.
Kikao hicho pamoja na masuala mengine, kitapokea taarifa za kina, kujadili na kufanya maazimio kuhusu hali ya siasa nchini.
Halikadhalika kikao hicho kitajadili kuhusu uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika katika kata 79 na jimbo moja la uchaguzi, kama ilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni.
Pichani, Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Mbowe akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Prof. Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. Kushoto kwa Mwenyekiti Mbowe ni Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara, John Mnyika.